Jumanne , 6th Jan , 2015

Miss Tanzania mwaka 2013 Happiness Watimanywa amewashukuru Watanzania kutokana na ushirikiano waliouonesha na kufanikisha ushiriki wake katika mashindano ya Miss World yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Miss Tanzania 2013/14 Happiness Watimanywa

Happiness amesema kutokana na ushirikiano aliopewa na Watanzania walimfanikisha kushika nafasi ya pili katika kipengele cha People's Choice nafasi ambayo ni ya heshima kubwa katika mashindano hayo ya urembo ya dunia.