Jumatatu , 14th Feb , 2022

Mahakama ya usuluhishi ya michezo (CAS) imetoa ruhusa kwa nyota  kutoka nchini Urusi, Kamila Valieva kuendelea kushiriki kwenye michezo ya baridi ya Olympiki 2022 inayoendelea mjini Beijing nchini China licha ya kushindwa kwenye vipimo vya afya alivyochukuliwa mnamo december 25, 2021.

(Kamila Valiela akiwa dimbani)

"Yupo huru kushiriki mana analindwa na sheria ya WADA kwa kuwa yupo chini ya miaka 16, kwani hayakuwa makosa yake maana bado yupo kwenye uangalizi wa wazazi wake" amesema katibu mkuu wa CAS, Matthieu Reeb.

Valieva mwenye miaka 15, ambaye ni nyota kwenye mchezo wa kuteleza kwenye barafu (skating) anaiwakilisha nchini ya Urusi kwenye michezo ya olimpiki ya baridi, alisimamishwa February 8, 2022 na shirika la kupinga madawa michezoni nchini Urusi (RUSADA) baada ya kutoka kwa majibu ya vipimo kuonesha alitumia madawa yasiyoruhusiwa michezo aina ya Trimetazidine alizotumia kwa ajili ya matatizo ya kifua (Angina).

Nyota huyo sasa atashiriki siku ya Jumanne Februari 15, 2022 kugombea medali ya dhahabu  kwenye michezo ya kuteleza kwenye barafu huku Wada wakiaanza kufanya uchunguzi kwa watu wanaomzunguka wakiwemo makocha, madaktari na wazazi wake  kujua kitu gani  kilisababisha kushindwa kwenye vipimo vya afya mwezi December 2021.