Kamanda wa Police mkoa wa Kagera SACP Brasius Chatanda amesema jeshi hilo limejipanga kuimarisha ulinzi na Usalama wakati wa uchaguzi huo na kuhakikisha wananchi wanapiga kura kwa amani na utulivu.
SACP Brasius Chatanda amesema kuwa mkoa utaendelea kuwa salama wakati na baada ya uchaguzi na kuwataka wananchi kutokuwa na hofu na kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
"Tumejipanga na sasa tumepokea magari matano yatatusaidia kwenye utendajikazi, zoezi la uchaguzi litaenda salama wananchi mjitokeze kupiga kura na niwahakikishie mkoa wa Kagera utakuwa na amani sasa, wakati wa uchaguzi na hata baada ya uchaguzi"