Alhamisi , 18th Dec , 2014

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo mkoani Arusha imemtunuku shahada ya heshima ya uzamivu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete.

Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo mkoani Arusha imemtunuku shahada ya heshima ya uzamivu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kukuza na uendelezaji wa sayansi na teknolojia hapa nchini.

Rais Dakta Kikwete ametunukiwa shahada hiyo ya heshima na mkuu wa chuo hicho makamu wa Rais Dakta Mohammed Gharib Bilal katika mahafali ya pili ya chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Nelson Mandela ambapo jumla ya wahitimu 106 wametunukiwa shahada zao kati yao wahitimu 93 wakitunukiwa shahada za uzamili na 13 shahada za uzamivu.

Akizungumza mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo Rais Kikwete amesema.

Awali akizungumza kwenye mahafali hayo mwenyekiti wa baraza la chuo hicho Profesa David Mwakyusa amesema hatua iliyofikiwa sasa ya ujenzi wa maabara ni muhimu sana katika kuendeleza sayansi na teknolojia nchini na kwamba upo umuhimu wa serikali kuwa na programu maalum ya kukuza masomo ya sayansi ili maabara hizo ziweze kutumika na kufikia malengo.

Mahafali hayo pia yamehudhuriwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Gate Chewingida ambaye anasema shirika hilo linatambua umuhimu wa chuo cha Nelson Mandela katika maendeleo ya nchi za Afrika na kwamba UNESCO itaendelea kuzijengea uwezo nchi za Afrika katika kufikia malengo.