Wanafunzi na walimu shule ya sekondari Binza Wilayani Simiyu walipopokea taulo za kike
Zoezi la mwisho la ugawaji limefanyika katika shule ya Sekondari Badi Wilayani Maswa mkoani Simiyu, ambapo walimu na wanafunzi wameeleza kufurahishwa na msaada huo wakiamini utasaidia kuondoa changamoto wakati wa hedhi na kufanikisha ndoto za wanafunzi wengi.
Katika awamu hii ya kwanza ya ugawaji iliyomalizika, Kampeni ya Namthamini imefanikiwa kuwaweka shuleni wanafunzi 800 kwa mwaka mzima, wakiwa na uhakika wa kuepukana na kadhia ya kukosa taulo za kike kwa kipindi hicho chote.
Tazama Video hapo chini