
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema mwanamke huyo Etina Silumba amemuua mume wake kwa kumkata kisogoni na kichwani na kitu kinachodhaniwa kuwa ni panga, na kisha kumvunja shingo na mguu wa kushoto.
Kamanda Msangi amesema kabla ya kutenda unyama huo usiku wa Jumatatu ilidaiwa mtuhumiwa alikuwa na ugomvi na marehemu mumewe, na polisi wanamshikilia mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Kamanda Msangi anatoa wito kwa wanandoa kutatua migogoro yao ya kimapenzi kwa njia ya kukaa meza moja ya mazungumzo, badala ya kuamua kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria.