Jumapili , 12th Sep , 2021

Mechi ya mkondo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali kati ya Yanga SC ya Tanzania dhidi ya Rivers United FC ya Nigeria imemalizika kwa Rivers United kushinda goli 1-0.

Katika mchezo huo ambao umepigwa leo Jumapili Septemba 12 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, timu zilitoshana nguvu katika dakika 45 za kwanza.

Katika kipindi cha pili timu zilianza kwa kushambuliana kwa zamu kabla ya Rivers United kupata goli la kuongoza kupitia kwa Moses Omoduemuke dakika ya 51.

Baada ya mchezo huo wa kwanza sasa mchezo wa mkondo wa pili utapigwa nchini Nigeria wiki mbili zijazo.