Jumatatu , 15th Dec , 2014

Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mtwara kimekiri kuwa upinzani umekuwa hasa maeneo ya mjini baada ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuonesha kuwa CCM imeshinda viti 58, wakati vyama vya upinzani vikiwa vimeshinda mitaa 53.

Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Mtwara kimekiri kuwa upinzani umekuwa mkubwa hasa maeneo ya mjini baada ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuonesha kuwa CCM imeshinda viti 58, wakati vyama vya upinzani vikiwa vimeshinda mitaa 53.

Akitoa taarifa ya matokeo hayo katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Shaibu Akweilombe amesema mitaa iliyoshindaniwa katika manispaa ya Mtwara mjini ni 111, na CCM imepita bila kupingwa mitaa 11 na mitaa 100 ilisimamisha wagombea.

Amesema pamoja na ukomavu huo CCM imeendelea kuongoza katika mitaa, vijiji na vitongoji katika mkoa huo.

Kwa upande wa vyama vya upinzani CUF imeshinda mitaa 36 sawa na asilimia 32, Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mitaa 16 sawa na asilimia 14 vingine ni NCCR Mageuzi mitaa 4 sawa na Asilimi 3.1 na TLP mtaa 1 asilimia 1.

Akiongea mara baada ya kupokea matokeo hayo mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani Lembakisye Shimwela amesema wananchi waliotegemewa kujiandikisha ni 43,000 na waliojiandikisha ni 32,000 ingawa bado hawajapata takwimu kamili za idadi ya wapiga kura waliweza kujitokeza kupiga kura.