![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2018/06/02/SINGIDAD UNITD.jpg?itok=5FjCoyzB×tamp=1527950824)
Hilo limebainishwa na Mkurungezi wa timu hiyo Festo Sanga muda mfupi baada ya mchezo wa fainali ambapo ameeleza kuwa wamezingatia ubora wa mwalimu huyo na uzoefu wake katika soka la Tanzania.
''Nadhani wote tunafahamu ubora wa kocha Hemed Morocco ambaye amefundisha timu ya taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa mafanikio makubwa hivyo bila shaka yoyote tumejiridhisha kuwa ni mwlaimu bora'', Sanga.
Hemed Morocco aliiongoza Zanzibar Heroes kufika fainali ya Kombe Ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) na kufungwa na wenyeji Kenya 3-2, mchezo uliopigwa Disemba 17, 2017.
Hans Van Pluijm ameiaga rasmi Singida United leo na ataanza kibarua chake ndani ya klabu ya Azam FC ambayo ameingia nayo makubaliano mwishoni mwa msimu wa ligi 2017/18 Mei 28.