Jumapili , 8th Aug , 2021

Kocha wa klabu ya AS Roma, Jose Mourinho amejikuta akitolewa nje ya uwanja wakati timu yake ya Roma ikimaliza mchezo wa kirafiki ugenini dhidi ya Real Betis ikiwa na wachezaji nane.

Kocha Jose Mourinho kwenye malalamiko dhidi ya mwamuzi

Wenyeji Real Betis walikuwa wanaongoza kwa mabao 3-2 hadi kufikia dakika ya 57 lakini wachezaji wa Roma walilalamika tukio la mfungaji Alex Moreno aliyeushika mpira kwenye mstari wa goli.

Katika mchezo huo, kiungo Lorenzo Pellegrini alipatiwa kadi ya pili ya njano, wakati kocha Mourinho pia akitolewa nje ya uwanja kwa kupinga maamuzi hayo ya refa.

Gianluca Mancini na Rick Karsdorp nao pia walijikuta wakilambwa kadi za njano za pili katika dakika za mwisho, wakati Betis ikifunga mara mbili na kushinda mabao 5-2.