
Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Daniel Masolwa
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Daniel Masolwa, jijini Dodoma na kusema kwamba shughuli za uchimbaji wa madini na mawe ziliongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha ukuaji hali iliyopelekea pato kupanda.
"Katika kipindi cha robo ya kwanza 2021, shughuli za uchimbaji madini na mawe ziliongoza kwa kuwa na kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 10.2 ikifuatiwa na Habari na Mawasiliano asilimia 9.1, uchukuzi na uhifadhi mizigo 9.0%, maji safi na majitaka 9.0%, huduma za kitaalam, sayansi na ufundi 7.8%, huduma zinazohusiana na utawala 7.4% na umeme 7.2%," amesema Masolwa.
Aidha, Masolwa amefafanua kwamba ukuaji wa Pato la Taifa katika kipindi hicho Masolwa amesema kuwa pato la Taifa katika robo ya kwanza ya mwaka 2021 ni asilimia 4.9 ukichangiwa na shughuli mbalimbali za kiuchumi zilizofanyika katika kipindi hicho.