Alhamisi , 5th Aug , 2021

Msanii wa filamu Patrick Kanumba amekana kuwahi kuwa kwenye mahusiano na Gigy Money kama ambavyo ilivyokuwa inazungumziwa mitandaoni kwamba wawili hao wana mahusiano ya siri.

Patrick Kanumba kushoto, kulia ni Gigy Money

Akijibu hilo kupitia EATV & EA Radio Digital, Patrick Kanumba amesema.

"Hapana sio kweli chanzo chake sijui imetokea wapi mimi nashangaa, sijawahi kuwa kwenye mahusiano naye kabisa hata hao watu wa mitandaoni sijui nao wanatoa wapi nashangaa".