Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe, akionesha chuma kilichotumika kumjeruhi Askari
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuvamiwa na kujeruhiwa askari wa barabarani namba H1619 John Charles lililopelekea wananchi wenye hasira kali kuingilia kati na kumuuwa muhusika kwa kipigo.
Aidha, Kamanda Mwaibambe amewataka wananchi wenye migogoro binafsi na Askari kuacha kujichukulia hatua mkononi badala yake watoe taarifa kituo cha polisi kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zinazostahiki.