Jumatatu , 14th Jun , 2021

Miaka ya hivi karibuni mambo mengi yamebadilika sana kwenye upande wa kiwanda cha muziki wa Tanzania.

Picha ni Mtayarishaji Abbah, Lady Jay Dee na Dogo Janja

Baada ya kupitia kipindi cha mpito pasipo kusikia wasanii wakiongelea taarifa za Extended Play (EP), Long Play (LP), Mixtape na Album huku kilio chao kilikuwa ni kudorola kwa soko.

Hali kwa sasa inavutia kwani tumeendele kushuhudia wanamuziki wengi wakiongelea habari za kuachia EP pamoja na Albums huku hata sokoni si haba kwani mitandao yaku-stream muziki imekuwa ikitoa records za mauzo ambayo kiasi fulani inavutia.

Kwa kipini cha miezi sita (Nusu ya mwaka) mpaka sasa kuna zaidi ya album 7 na EP kibao na za moto kweli ambazo zipo sokoni.

Baadhi ya Album ni;

The Evolution – Mwezi Februari, 2021 mtayarishaji wa muziki Abbah Process aliachia album yake ya kwanza yenye nyimbo kali zisizopungua 16 ambazo zimefanikiwa kutikisa sokoni kwa streams.

Asante Mama – Album hii ya Dogo Janja ambayo ina jumla ya nyimbo 11 ilitoka Mei, 2021 huku nyimbo 9 akiwa amewashirikisha wasanii wa jinsia ya kike pekee ambao ni Linah, Rosa Ree, Khadija Kopa,Lulu Diva, Maua Sama, Mimi Mars huku ikiwa ni ya pili kwake na mpaka sasa imefikisha streams laki 5 kupitia Boomplay Music.

20 – Hii ni album ya 8 kwenye career yake ya muziki mkongwe huyu Lady Jaydee ambayo ina nyimbo 20, na kushirikisha wasani kama Domokaya, Niniola, Mr Blue, Belle 9, Maunda Zorro nawengine wengi.

Kwenye mtandao wa Boomplay Music 20 imesikilizwa na watu zaidi ya laki 4.

Digala – Pia ni moja kati ya album kali kutoka kwa Legend Domokaya ambayo imehusisha wasanii wakubwa kama G Nako, Top In Dar (T.I.D), Linex na Malkia Karen huku jumla ya nyimbo 12 ndizo zinazopatikana humo.

Air Weusi – Ilikuwa ni ahadi ya muda mrefu kutoka kwao Weusi juu ya ujio wa album yao na hatimaye Machi 12, 2021 ilitoka Air Weusi huku ikiwa na nyimbo 14 na mpaka sasa imesikilizwa na watu zaidi ya laki 2 kwenye mtandao wa kusikilizia na kupakulia muziki wa Boomplay Music.

Hii imebainika kuwa mahitaji ya wanamuziki yamekuwa makubwa ya kuacha album baada ya ongezeko la wasanii wengi ambao wanaendelea kuandaa na wanatarajia kuziachia mwaka huu kama Harmonize, Alikiba, Maua Sama, Marco chali, S2kizzy na wengine kibao huku utaratibu wa single ukiwa umepungua kasi katika msimu wa hivi karibuni .