Jumanne , 25th Mei , 2021

Msanii Twenty Percent amejibu madai ya kuonekana kama mtu ambaye analalamika sana kwenye interview zake ambazo amekuwa akihojiwa.

Picha ya msanii Twenty Percent

"Kwenye maongezi unaweza ukaongea mwingine akapokea tofauti, naweza nikazungumza vile ambavyo naona ila mwingine akaweka fikra ya kuona kwamba 20 Percent analalamika, mwingine atanitazama kama nimenyanyasika mwingine anaona kama nawapiga watu beat au kutaka msaaada".

Pia amezungumzia ishu ya trending ya muziki wa sasa kwa kusema "Muziki mzuri ni ule unaoishi kwa muda mrefu kwenye mioyo ya watu na sio ambao unaishi kwa ajili ya kiki au neno lililotumika, maana kuna wengine wanaandika nyimbo kupitia neno lililo-hit kwa siku kadhaa".