Jumatatu , 24th Mei , 2021

Kocha wa FC Barcelona Ronald Koeman atakutana na Rais wa klabu hiyo Joan Laporta, ili kujadili juu ya mustakabali wake wa kuendelea kufanya kazi klabu hapo lakini pia maswala mbali mbali ya usajili kuelekea msimu ujao wa 2021-22.

Kocha Ronald Koeman

Inaripotiwa kuwa kocha huyo raia wa Uholanzi bado hajaju hatma yake kama atasalia klabu hapo au atafutwa kazi baada ya kuukosa tena ubingwa wa Li Kuu La Liga, hivyo atakutana na Rais wa klabu Joan Laporta ndani ya wiki hii, ili kujua hatma yake lakini pia kupanga mipango mbali mbali ya usajili kuelekea msimu ujao wa mashinda.

Taarifa kutoka Hispania zinadai kuwa kocha huyo hata kama akisali ndani ya kikosi hicho basi atalazimika kuuza wachezaji taklibani kumi (10) ili kuongeza pesa ya bajeti ya usajili, katika maboresho ya kikosi.

FC Barcelona imeukosa ubingwa wa ligi kuu nchini Hispania msimu huu La Liga kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kumaliza nafasi ya tatu (3) nyuma ya Mabingwa Atletico Madrid na Real Madrid waliomaliza nafasi ya pili lakini pia msimu wa 2019-20 walimaliza nafasi ya pili.

Na katika sakata la Lionel Messi klabu hapo kama ataondoka au atabakia bado haijajulikana, lakini inaaminika endapo kama Barca itafanikiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji Sergio Kun Aguero kutoka Manchester City basi Messi anaweza kusalia. Messi na Aguero wote ni raia wa Argentina na ni marafiki wa karibu sanaa.