
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Luis Suarez akilia kwa hisia baada ya kuisaidia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania.
Suarez aliyekua na mhemko alirudisha akili yake katika kitendo cha kufukuzwa bila huruma na Barcelona ndipo alipo dondosha chozi la furaha.
Raia huyo wa Uruguay amesema Barcelona hawakumthamini kabla ya kumuondoa msimu uliopita majira ya joto, lakini wakati huo Atletico Madrid walimfungulia milango na kumkaribisha, hivyo muda wote atajisikia faraja kwa klabu hiyo kumuamini na kumpa nafasi.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33, aliangua kilio kwa hisia kali wakati mchezo dhidi ya Valladolid ulipomalizika na Atletico Madrid kufanikiwa kutwaa ubingwa wa LaLiga baada ya kupata ushindi wa magoli 2 kwa 1.
Pia Suarez aliongeza kusema: “Nina hakika Lionel Messi anafurahi kwangu kama rafiki, sababu ilikuwa hali ngumu ambayo ilibidi niipitie kwa jinsi nilivyo tendewa”(na Barcelona)