Jumapili , 16th Mei , 2021

Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Rufaa Mkoa wa Songwe, Dr Lulandala amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa wakinamama wanaoenda kupata huduma ya kujifungua na kutozwa pesa kiasi cha Tsh 200,000 kwa wanaojifungua kwa Operation na Tsh 150,000 kwa wanaojifungua kawaida.

Mganga Mkuu wa Hospitali Teule ya Rufaa Mkoa wa Songwe, Dr Lulandala

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Dr Lulandala amewataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo kwani si za kweli na ikiwa kuna mwananchi ametozwa kiasi hicho anatakiwa kutoa taarifa ili swala hilo lichukuliwe hatua kikamilifu.