Mwanamke akiwa anajishughulisha kutengeneza Pombe za Kienyeji.
Akizungumza wakati wa upokeaji wa kupokea msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea yatima cha Cornel Ngaleku mkuu wa kituo hicho Sister Ritha Masawe amesema tatizo la ulevi katika wilaya hiyo limesababisha hata kuhujiwa kwa baadhi ya vitu kituoni hapo kutoka kwa vijana waliojiingiza katika matumizi ya pombe hizo wakiwa hawana shughuli za kufanya.
Sister Ritha ameongeza kuwa hata watoto wengi katika wilaya hiyo wanakosa malezi bora kutoka kwa wazazi wao ambao wengi wao wamejiingiza katika uzalishaji na unywaji wa pombe hizo kiasi cha kufanya na watoto pia kujiingiza katika matumizi ya pombe wakiwa katika umri mdogo na kurudisha nyuma uchumi wa eneo hilo.
Bi. Ritha ameongeza kuwa hali hiyo pia imepelekea vijana wengi kujiingiza katika makundi ya kihalifu katika eneo hilo ili kujitafutia pesa isivyo halali na kusema yote ni matokeo ya viwanda hivyo vya pombe za kienyeji.