Soko la vinyago lililoko karibu na ofisi ya CCM wilaya ya Arusha limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia tarehe 18 Novemba 2014 na kusababisha hasara ya mabilioni ya fedha.
Wananchi na wafanyabiashara ambao vibanda na mali zao zote zimeteketea wamesema walianza kupata taarifa za moto huo usiku wa kati ya saa tatu na saa Nne na walivyofika walikuta kila kitu kimeteketea.
Wananchi hao wamesema inakuwa vigumu kubaini chanzo cha moto huo kwani katika eneo hilo ambalo linamilikiwa na chama cha mapinduzi (CCM) hakuna umeme wala chanzo chochote cha moto.
Aidha wananchi wameiomba serikali na vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi na kuchukua hatua ya kuwasaidia kwani ni janga kubwa kwao hasa ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa wanaendesha biashara zao kwa kutegemea mikopo