Jumatatu , 17th Nov , 2014

Rapa Mabeste baada ya kuachia video mpya ya ngoma yake ya 'Nishauri', amefunguka juu ya lebo yake mpya ambayo yeye ndio boss wake, akishirikiana na mkewe wakiwa tayari na msanii ambaye hivi karibuni watamtambulisha katika tasnia ya burudani.

msanii wa muziki wa bongofleva Mabeste akiwa na mkewe

Mabeste amesema kuwa kwa sasa ngoma yake itakayotoka inakwenda kwa jina 'Beautiful' na itakuwa chini ya uongozi huu Dole Entertainment, nafasi nyingine nzuri ya kuonyesha ladha mpya na Mabeste akiwa amebadilika kwa kiasi kikubwa.