Kushoto ni wachezaji wa Simba SC na kulia ni Mohammed Dewji na Hamisi Kigwandalla
Mo Dewji ameweka wazi hilo leo Novemba, 25, 2020 kwa kuomba radhi kwa pale alipomkosea Kigwangalla wakati wakijibizana juu ya Bilioni 20 za uwekezaji Simba. Lakini pia ameweka wazi kuwa ameshasamehe kwa pale alipokosewa na Kigwangalla, huku akieleza nia ilikuwa ni kuijenga Simba SC.
Nia njema ni tabibu, nia njema ni ibada. Sote tuna mapenzi ya dhati na Simba, hata tulipokwazana ilikua katika nia njema kwenye maendeleo ya timu yetu. Naomba radhi nilipokosea na mimi uliponikosea nishasamehe. Tuijenge Simba pamoja sasa #NguvuMoja pic.twitter.com/czLfNSlprO
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) November 25, 2020
Hivi Karibuni Kigwangalla pia aliweka wazi kuhusu kumaliza tofauti hizo na kueleza kuwa yeye ameshasamehe na sasa washirikiane kujenga klabu.