Mkuu wa TAKUKURU mkoani Geita Leonidas Felix
Akizungumzia tukio hilo Oktoba 10,2020, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Geita Leonidas Felix amesema mfanyabiashara huyo alimkopesha mwalimu Adela, kiasi cha shilingi za Kitanzania laki saba na kumlazimisha kurejesha milioni saba baada ya kugundua kuwa mwalimu huyo amelipwa kiinua mgongo baada ya kustaafu.
‘’Tulifanya upekuzi kwa huyu mtuhumiwa na alikutwa na kadi 64 za benki za wateja wake ambao ni wakopaji’’, amesema Leonidas Felix.
Aidha mkuu huyo amesema mfanyabiashara huyo alitumia njia za vitisho ambapo alimtaka kulipa milioni saba ambayo ni sawa na asilimia 900 ambapo amesema hiyo ni dhuluma na kwamba TAKUKURU haitavumilia vitendo hivyo.
Baada ya kutoa Milioni tano na laki tano katika awamu ya kwanza, mfanyabiashara huyo atamalizia milioni moja na laki tano ili kumalisha Milioni saba.