Alhamisi , 8th Oct , 2020

Mshambuliaji wa Chelsea, Olivier Giroud amekuwa mfungaji bora namba mbili wa muda wote wa timu ya taifa ya Ufaransa akimpiku Michel Platini.

Giroud amebakiza mabao 9 kumfikia kinara wa ufungaji wa muda wote wa Ufaransa Thierry Henry mwenye mabao 51

Giroud alifunga mabao mawili katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Ukraine, mchezo ambao Ufaransa iliibuka na ushindi wa mabao 7-1.

Mabao hayo mawili ya dakika 24 na 33 yamemfanya Giroud afikishe mabao 42 katika mechi 100 alizoichezea timu yake ya taifa.

Kwa idadi hiyo ya mabao, Giroud amebakiza mabao 9 kumfikia kinara Thierry Henry mwenye mabao 51.

Gwiji wa Ufaransa, Michel Platini aliyekua akishika nafasi ya pili hivi sasa ameporomoka hadi nafasi ya 3 akiwa na mabao yake 41 .

Mabao mengine ya Ufaransa katika ushindi huo yalifungwa na Eduardo Camavinga dakika 9, Corentin Tolisso dakika 65, Kylian Mbappe dakika 82 na Antoine Griezmann dakika 89 na bao moja Vitaliy Mykolenko's wa Ukraine alijifunga dakika ya 39 Bao pekee la Ukraine lilifungwa na Viktor Tsyhankov dakika ya 53.

Kikipigo cha bao 7-1 ni kikubwa zaidi katika historia ya Ukraine ambayo kwa sasa inanolewa na nyota wa zamani wa AC Milan na Chelsea Andriy Shevchenko