Jumatano , 7th Oct , 2020

Kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Mario Gotze amejiunga na klabu ya PSV ya Uholanzi.

Mario Gotze akitambulishwa PSV

Shujaa huyo wa kombe la Dunia mwaka 2014 alikuwa huru mara baada ya kumaliza mkataba na Borussia Dortmund aliyojiunga nayo mwaka 2016 akitokea Bayern Munich

''Ninafanya mazoezi binafsi kila siku, najianda vizuri kukabiliana na changamoto mpya kabla ya kwenda kujiunga na mazoezi ya pamoja ya timu, nina umri wa miaka 28 najiona nina muda bado wa kufanya makubwa katika soka'' alisema Gotze

Gotze alikuwa shujaa wa Taifa la Ujerumani katika fainali za kombe la dunia 2014 Brazil, baada ya kufunga goli pekee dhidi ya Argentina katika mchezo wa fainali uliomalizika kwa ushindi wa goli 1-0 ambapo Ujerumani walitwaa ubingwa wa kombe la Dunia.

Akiwa na Bayern Munich, Gotze alifunga magoli 22 katika michezo 73 wakati alipokua na Borussia Dortmund aliwafungia magoli 13 katika michezo 75 , vilevile aliifanya vyema akiwa na timu ya Taifa ya Ujerumani aliyoifungia magoli 17 katika michezo 65.