Akizungumzia zoezi hilo Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo Dkt. Laurent Lemeli, amesema kuwa taasisi hiyo imekuwa ikifanya upasuaji kwa watoto wasiopungua wa nne kila siku.
Azim Dewji ni mmoja wa wadau waliofanikisha zoezi hilo la upasuaji kwa watoto hao, amewaomba Watanzania kujitoa kusaidia matibabu kwa watoto hao ambao wengi wao hutoka katika mazingira magumu.
EATV imezungumza na moja kati ya wazazi wenye mtoto matatizo ya aina hiyo na kuelezea changamoto wanazokutana nazo wakina mama katika malezi ya Watoto wa iana hiyo. "Changamoto kubwa ni malezi yanayotokana na hyali yao na jamii nyingi imekuwa ikiwatenga ikiwemo kuibuka kwa maneno mengi yakihusishwa na imani za kishirikina"