Mwenyekiti wa soko hilo Mbaraka Kilima amesema licha ya idadi kubwa ya watu wanaotumia soko hilo lakini wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha soko linakuwa katika mazingira ya usalama kwa afya za watu kwa kuzingatia usafi wa mazingira..
"'Mwitikio umekuwa mkubwa zaidi ya mipango yetu na hii ni kutokana na mahitaji mikakati iliyopo ni kuhakikisha tunaboresha miundombinu ili kuweza kukidhi mahitaji ya wateja"
Kwa upande wake katibu wa wadau wa soko hilo Nassoro Mbaga ameiomba serikali kuangalia utaratibu mpya utakaosaidia kupunguza idadi hiyo ya watu kwa kuwa kuna miundombinu mingine ya soko haihitaji matumizi makuhwa.