Jumanne , 25th Aug , 2020

Kuelekea siku ya mwananchi August 30, Staa wa BongoFleva Harmonize amefunguka kusema yeye ni mwananchi na timu yake ni shabiki wa timu ya Yanga pia hataki mashabiki wake wa muziki wajigawe kwa sababu anaishangilia timu hiyo.

kushoto ni msanii Harmonize, kulia ni logo ya timu ya Yanga

Harmonize amesema mambo ya mpira yasichukuliwe kama mambo binafsi kwani mpira sio vita kwamba anashangilia Yanga basi mashabiki wake ndiyo wajigawe, pia ameahidi jinsi atakavyoshuka siku ya tukio hilo watu hawataamini.

"Mimi ni mwananchi timu yangu ninayoishabikia ni Yanga, kwenye michezo na hakuna hisia ngumu kwamba nikishangilia timu fulani eti mashabiki wangu wajigawe pia mpira sio vita, nia yetu ni kuusogeza mpira mbele wala sio uadui, ila ninachowaahidi siku ambayo nitashuka pale uwanja wa Mkapa hamtaamini" amesema Harmonize 

Pia Harmonize ametunga wimbo maalum kwa mashabiki wa Yanga kuelekea siku ya Wananchi ambayo itakuwa August 30.