Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa na mabomu manne ya kivita ambayo yanasadikiwa ni miongoni mwa mabomu yanayotumika katika vitendo vya uhalifu yaliyotokea sehemu mbali mbali nchini.
Kamishna wa jeshi la polisi Zanzibar CP Hamdani Omar Makame amethibitisha kukamatwa kwa mtu huyo ambaye kwa mujibu wa jeshi hilo mtu huyo amekiri kuwa anajishughulisha na mtandao wa kuagiza,kuingiza na kuhifadhi mabomu yakivita ya kurushwa kwa mkono na mabomu hayo yalikuwa matano na polisi wamesema huenda moja ya hilo likawa ndilo lilotumika Darajani na kuongeza kuwa mtandao huo unausihwa na matukio kadhaa nchini.
Hata hivyo Kamishna Hamdani amesema kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye hatahivyo amekataa kumtaja jina na mazingira ya ukamataji wake amesema kuwa hahusiani na imani ya kidini na polisi inamshughulika mtu kisheria kutokana na kosa lake kwa mujibu wa sheria za nchi na siyo Imani za kidini.
Wakati polisi imekataa kutoa taarifa yoyote kuhusu mtuhumiwa huyo, jeshi hilo limesema hakuna kosa lolote la kisheria endapo mtu akipelekwa nje ya Zanzibar kwa kosa la ugaidi huku akisema bado polisi inaendelea na upelelezi wa tukio hilo kama ni la Zanazibar au ni mtandao wa ugaidi wa nchi nzima.