Alhamisi , 23rd Oct , 2014

Michuano ya Mieleka Klabu bingwa Taifa inatarajiwa kufanyika Desemba 19 mpaka 24 mwaka huu Mkoani Tanga.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa Chama cha Mielekeka nchini AWATA, Bernard Mwakalukwa amesema mpaka sasa wameshatuma barua kwa vilabu shiriki ambapo vinatakiwa kuhakiki ushiriki wao wiki mbili kabla ya michuano hiyo.

Mwakalukwa amesema wameamua kuipeleka michuano hiyo mkoani humo, ili kuweza kukuza mchezo huo na kuweza kupata washiriki mbalimbali wa mchezo huo watakaoweza kushiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.