
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba.
Profesa Lipumba ameyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara yake Visiwani Pemba, ambapo alisema chama cha siasa kupora ofisi za chama kingine cha siasa ni kuvunja sheria ya vyama vya siasa.
''Ni bora ofisi za majengo ya CUF waliyoyahodhi na kuyapaka rangi za ACT Wazalendo wazirejeshe kwani hali hiyo inaweza kuwasababishia adhabu kubwa dhidi ya kupora ofisi hizo'', amesema.
Aidha Profesa Lipumba amesema vyama vya siasa visiwe chanzo cha uadui na badala yake wafanye siasa za kisasa na kushindana kwa hoja kuwa nani anayeweza kutumia wananchi vizuri zaidi kwani katiba ya umoja wa kitaifa inawapa fursa ya kuweza kutekeleza Sera zao.
Zaidi Tazama Video hapo chini