Picha ya kikosi cha Simba SC 2019/2020
Simba SC imetangaza jambo hilo kupitia katika ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo wameandika,
"Unaikumbuka saa 7 mchana, tukutane Jumamosi hii Mei 23, 2020. Historia mpya kwa klabu kaa tayari NguvuMoja"
Sasa kama unaikumbuka Saa 7 Mchana ilikuwa ni sera mpya ya Simba SC, ambapo walikuwa wanatumia wakati huo kutambulisha na kuwasaini wachezaji wao wapya, matukio makubwa au jambo lolote lililohusu klabu hiyo.