Jumamosi , 7th Mar , 2020

Moja kati ya vitu vinavyosubiriwa kwa hamu kwa mashabiki wa soka hapa Tanzania ni kuelekea mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba utakaopigwa  siku ya Machi 8, 2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Msanii Dully Sykes

EATV & EA Radio Digital, imempata msanii mkongwe wa BongoFleva Dully Sykes ambaye ametoa maono yake kuelekea mchezo huo ambapo amesema yeye ni shabiki wa Yanga, na mashabiki wa Simba waache kuwasumbua kwa sababu wana maneno sana.

"Unajua mimi nimezaliwa K.Koo na watu wengi wa kule ni mashabiki wa Yanga na familia yangu ndiyo waasisi wa CCM ambao wote ni Yanga, wasikisumbue kikosi chetu halafu mashabiki wa Simba wana maneno mpaka sisi tunashindwa kuhimili na kuvuka mipaka, watuache na wanyamaze kimya" amesema Dully Sykes