Ijumaa , 28th Feb , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amefanya ziara ya kushtukiza ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti wa BAKWATA unaojengwa eneo la Kinondoni, Dar es Salaam, kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco.

Kushoto ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubeir, katikati ni Rais Dkt John Magufuli, kulia ni Sheikh Mkuu wa Dsm , Alhad Mussa Salum.

Ziara hiyo ameifanya leo Februari 28, 2020, ambapo ameongozwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir, Rais Magufuli amejionea kazi za ukamilishwaji wa Msikiti huo zikiendelea kukamilishwa.

Kwa upande wake Sheikh Aboubakar Zubeir, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa Msikiti huo, ambao ujenzi wake umefikia asilimia 97.