Alhamisi , 4th Dec , 2025

Sheria hiyo mpya inawataka watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kuwa na akaunti katika majukwaa kama TikTok, Facebook, YouTube na Instagram.

Katika kulinda usalama wa watoto mtandaoni na kupunguza madhara ya kiafya na kijamii yanayoweza kusababishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii katika umri mdogo nchini Australia, kampuni ya Meta imeanza kuondoa akaunti za vijana walio chini ya umri wa miaka 16 kutoka kwenye mitandao yake ya kijamii.

Sheria hiyo mpya inawataka watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kuwa na akaunti katika majukwaa kama TikTok, Facebook, YouTube na Instagram.

Hatia hii itaifanya Australia kuwa taifa la kwanza duniani kutekeleza marufuku ya aina hii kwenye mitandao ya kijamii, agizo ambalo litatekelezwa kuanzia Desemba 10, ambapo kampuni zote zinazotoa huduma hizo zitakabiliwa na adhabu ya faini hadi A$49.5 milioni (sawa na takriban US$33 milioni au £25 milioni) endapo zitashindwa kuchukua “hatua zinazofaa” kuhakikisha watoto walio chini ya umri wa miaka 16 hawafungui akaunti.

Meta, kampuni mama ya Facebook, Instagram na Threads, ilitangaza mwezi uliopita kuwa imeanza kuwafahamisha watumiaji wenye umri wa kati ya miaka 13 na 15 kwamba akaunti zao zitaanza kufungwa kuanzia Desemba 4, 2025. Hatua hiyo itaathiri takriban watumiaji 150,000 wa Facebook na zaidi ya akaunti 350,000 za Instagram nchini humo.