Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe
Taarifa hiyo imetolewa leo Februari 28, 2020, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Hamphrey Polepole, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
"Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa, imeadhimia kwa kauli moja kumfukuza Bernard Membe uanachama wa CCM, uamuzi huu umekuja baada ya taarifa zake ndani ya chama kuonesha mwenendo wake tangu mwaka 2014, ambapo alishawahi kupata adhabu zingine ambazo zingeweza kumsaidia kujirekebisha lakini imeonekana sivyo" amesema Polepole.
Membe pamoja na Makatibu Wakuu wastaafu, miezi kadhaa nyuma waliibua mijadala mitandaoni baada ya sauti zao kuvuja, wakizungumzia uwepo wa mpasuko ndani ya CCM.

