Picha ya Piere Likwidi
Piere Likwidi amesema hayo wakati wa onyesho wa tuzo hiyo ya Kimataifa ya Kizibo Cha Dhahabu (IGCA), iliyopewa kampuni ya TBL kutoka Ulaya ambayo ina kilo 16.01 za dhahabu yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.
"Hii ni dhahabu tupu ambayo TBL wameshinda zawadi hii kutoka Ulaya ambao wametuona sisi tunafaa na wanywaji wazuri wa gambe, halafu tunyweni gambe linalipa jamani kwanza linakimea kizuri kunywa na wewe ufaidi kama mimi ninavyofaidi" amesema Piere Likwidi.
Onyesho la zawadi ya tuzo hiyo ya dhahabu kutoka TBL, litaendelea kupitishwa mitaani na leo watakuwa maeneo ya Karume na Buguruni wilayani Ilala, jijini Dar Es Salaam.

