Alhamisi , 27th Feb , 2020

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Katibu wa CCM Tawi la Jamhuri kata ya Daraja mbili, Aron Kivuyo, kwa ajili ya upelelezi kufuatia tuhuma za ubakaji na kumtia mimba mwanafunzi zinazomkabili.

Mikono iliyofungwa Pingu

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital leo Februari 27, 2020, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arumeru Denis Zacharia, amesema kuwa Kivuyo alikamatwa siku ya juzi ya Februari 25 akiwa ofisini kwake.

"Mimi walinipigia juzi wakati anachukuliwa na akakimbia kwa Katibu wake kumuambia kuwa Polisi wameagizwa wamkamate, ni suala la mimba na inatakiwa uthibitisho wa daktari kwa sababu yeye anakataa tuhuma hizo na hawajampa dhamana hadi wachukue maelezo yake kwanza" amesema Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru.