Jumanne , 24th Dec , 2019

Abiria wanaolekea Mkoa wa Iringa na baadhi ya Mikoa ya jirani wamekwama katika barabara ya Mlima Kitonga kufuatia Lori kupata ajali ya katikati ya barabara hiyo na kupelekea magari kushindwa kusafiri.

Lori lililopata ajali katika Barabara ya Mlima Kitonga kulekea mkoani Iringa.

Akizungumza na EATV na EA Radio Digital moja ya shuhuda wa ajali Habib Hanta amesema ajali hiyo imetrokea majira ya saa 8 Mchana, na kupelekea na kupelekea adha kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Aidha amesema mpaka sasa juhudi za kuliondoa Lori hilo ili waanz kupita bado zinaedelea.

Bado tunaendelea kufanya juhudi za kumtafuta RPC wa Mkoa wa Iringa Juma Bwire kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo.