Jumatatu , 22nd Sep , 2014

Rapa Izzo Business, ameweka wazi kuwa kazi ambayo inatarajia kutoka kwake kwa sasa, Video ya Walalahoi, imemgharimu kiasi cha shilingi milioni 1 na laki 3, na kwa kiasi hicho tu ameweza kufanya kazi yenye kiwango cha hali ya juu.

msanii wa bongofleva nchini Tanzania Izzo Bizness

Rapa huyu ameiambia eNewz kuwa kazi hii ndani yake imeongelea mambo mengi sana ambayo video yake itakua inayagusia pia, kitu ambacho kimesababisha ikachukua muda zaidi kuitengeneza ikiwa chini ya muongozaji Nick Dizzo.