RC Makonda na Askofu Gwajima
Akizungumza leo Septemba 17 na EATV&EA Radio Digital, Askofu Gwajima amesema kuwa, yeye binafsi yuko tayari kufanya hivyo kwa sababu neno la Mungu linapaswa lihubiriwe maeneo yote na liwafikie watu wote.
''Injili ya Yesu inatakiwa ihubiriwe kila mahali, iwe kwa wavuta bangi, iwe kwa wanaokunywa Pombe, alichokisema RC ni kile kimeandikwa kwenye Biblia, hivyo ni jambo zuri watu kuhubiriwa habari za Yesu ili wasije kusema hawakusikia, na mimi niko tayari ukiniita mahali kwamba nije nihubiri, naenda popote pale'' amesema Gwajima.
Makonda alitoa kauli hiyo Septemba 8, 2019, wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtume Mwamposa na aliahidi kutoa kibali kwa mtumishi yeyote, atakayekuwa tayari kueneza Injili katika maeneo hayo.
