Jumamosi , 10th Aug , 2019

Baada ya kutokea kwa ajali ya Lori la mafuta na kuwaka moto mkoani Morogoro, ambayo imesababisha zaidi ya watu 60 kupoteza maisha, wasanii wameeleza kuguswa na msiba huo.

Picha inayotumika zaidi mtandaoni kutoa pole.

Kupitia mitandao ya kijamii, watu maarufu kutokea katika sekta mbalimbali wameonyeshwa kuguswa na tukio la ajali hiyo na kuandika jumbe mbalimbali za pole na faraja kwa wahanga.

Barnba Classic  "Mungu Awape Uvumilivu na awaponye majeraha waliyopata ndugu zetu na Familia za watu wa morogoro, Poleni sana Mungu ashindwi kitu amewataka waja wake wakaje kwakwe na ndo alichagua njia hi iwe kwao Cha msingi maombi na Sara zetu zikawe Pepo na makazi mema kwao milele Amina".

Mwasiti  "morogoro jamani jamani jamani dah watu wamekufa kama utani.tuwe makini jamani sio kila kitu kina kimbiliwa,Vingine ni hatari, mwenyezi awalaze pema wapendwa wetu waliotangulia".

Jonas Mkude20   "PRAR FOR MOROGORO"

Professor Jaytz  "Ndugu zetu wapumzike kwa AMANI, AMINA"

Shilole   "Mungu azilaze roho za ndugu zetu mahali pema peponi"

Mo Dewji  "Inna lillahi wa inna ilaihi raji'un, Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, na awasimamie wanaohusika kwenye shughuli za uokoaji. Tuwaombee ndugu zetu. Mungu awape nguvu na subira wakati huu".

Billnass "So Sad...Morogoro Mwenyezi...Mwenyezi Mungu awape Nguvu ndugu Jamaa na wafiwa wote!! Awape nafuu Majeruhi Wote pia Awalaze pema peponi ndugu zetu wote waliotutangulia"

Amber Lulu  "Napenda kuchukuwa nafasi hii kuwapa pole ndugu zetu wa morogoro mungu awasimamie kipindi hichi kigumu"

Haji Manara  "Tuwaombee na Majeruhi wote wa ajali hii kubwa wapone haraka".