
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi, Rashid Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na kusababisha kifo cha mtoto huyo, aliyekuwa amebebwa na mama yake mgongoni Felister Nyerere ambaye kwa sasa ni majeruhi.
"Ni kweli kuna familia imegongwa walipokuwa wakitembea kwa miguu na katika ile ajali bahati mbaya mtoto wa miezi 8, ambaye alikuwa amebebwa na Mama yake amefariki Dunia, kutokana na aina ya ajali yenyewe, lakini ndugu wengine ni majeruhi na sasa wapo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi".
Kwa upande wake Baba Mzazi wa familia hiyo George Luchanganya ameeleza, kusikitishwa kwa kuondokewa na mtoto wake wa miezi 8, huku mke na mtoto wa miaka 2 wakiwa mahututi na kupatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, ambapo ametoa wito kwa Serikali kuandaa sheria kali kwa madereva wanaoendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani.