
Hilo limebainishwa leo Julai 17 na Kaimu Katibu wa baraza hilo Onesmo Kayanda mara baada ya kumaliza kikao cha ndani kilicholikutanisha baraza na wasanii, hao kwa lengo la kujadiliana masuala ya tasnia nzima ya sanaa.
''Ni kikao cha baba na mtoto, tunawekana sawa katika Tasnia ya Sanaa, kwa sababu wenzetu wamekuwepo kwenye sanaa kwa muda mrefu, lakini walikuwa hawajatambuliwa, walikuwa hawajasajiliwa, hivyo wanapaswa kusajiliwa'' amesema Kayanda.
Kwa upande wake mwanasheria wa BASATA Onesmo Ndinga, akizungumzia suala la Irene kuwarushia pesa waandishi wa habari, amesema wao hawajamuita kwa ajili ya kumshtaki ama kumpeleka Mahakamani, ila wao walimuita kwa lengo la kutimiza baadhi ya vigezo, ambavyo walikuwa hawajatimiza kwa mujibu wa sheria.
Mapema leo Uwoya na Steve Nyerere walifika ofisi za BASATA na kuingia kwenye kikao na wal=ipotoka waliomba msamaha mbele ya waandishi wa habari.
Tazama Video hapa chini Uwoya na Steve wakiongea baada ya kikao