Jumatano , 26th Jun , 2019

Serikali ya Jamhuri ya Kenya imewahakikishia usalama raia wa kigeni wanaotoka nje ya nchi, ambao wako nchini humo kwa ajili ya kufanya biashara ambapo wameeleza Kenya itaendelea kushirikiana na mataifa mengine.

Msimamo huo wa Kenya umetolewa kupitia taarifa ya Msemaji wa Serikali, Cyrus Oguna, kupitia video iliyoonekana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha Mbunge Jaguar akiwapa masaa 24 raia wa kigeni waishio Jimbo la Starehe, na kueleza si msimamo wa Serikali hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa "tunawaeleza kwamba maneno yanayozungumzwa kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii si msimamo wa Serikali hiyo, na wala hayana tija katika ulimwengu huu wa utandawazi."

"Mwisho Serikali ya Kenya inawahakikishia ulinzi na usalama raia wa kigeni wanaoishi Kenya na waendelee na biashara zao Wakenya wanaupendo sana." imesema taarifa hiyo

Jana jioni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema walizungumza na Ubalozi wa Kenya na kuwataka Watanzania waishio Kenya waendelee na shughuli zao kama kawaida.