Jumamosi , 22nd Jun , 2019

Akiwa bado anaandamwa katika mitandao ya kijamii baada ya kudaiwa kuvunjika kwa uhusiano wake na msanii mwenzake, Juma Khalid ‘Jux’, staa wa Bongo Flava, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema kuwa hawezi kumzuia mtu kusema chochote juu yao. 

Vanessa akiwa na Jux.

Vee Money amesema kwamba hawezi kuwazuia watu kusema kile ambacho wanajisikia katika mitandao ya kijamii kwa kuwa ni kawaida kwa binadamu kuongea anachokisikia.

Siku zote anayeujua ukweli ni mhusika mwenyewe. Mengi yanazungumzwa lakini kikubwa mimi naangalia kazi tu" amesema Vanessa.

Vanessa na Jux wameingia katika mijadala mtandaoni kutokana na madai yanayosambaa kuwa wamemwagana, huku wao hakuna aliyethibitisha juu ya tuhuma hizo.