Jumatatu , 1st Sep , 2014

Msanii Bebe Cool pamoja na mdau mkubwa wa muziki Uganda, Shaka Mayanja wamefanya vita ya maneno kwa njia ya mtandao kuhusiana na mtunzi halisi wa wimbo unaofanya poa sasa kutoka kwa Bebe Cool 'Love You'.

msanii wa muziki wa nchini Uganda Bebe Cool

Vita hii imeanza pale Mayanja alipotoa maoni yake kuwa baada ya kusikia wimbo huu moja kwa moja, akajua kuwa Bebe Cool ameandikiwa na msanii chipukizi anayekwenda kwa jina Estah, maoni ambayo Bebe ameyachukulia kama choko choko.

Baada ya kuona maoni haya, katika majibu ya Bebe Cool amemtaka Mayanja kuacha kutafuta sababu ya kumshusha chini, huku akidai kuwa yeye ndiye aliyeandika sehemu kubwa ya wimbo huu.