
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage
Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage leo Jijini Dar es Salaam katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa vyama vya siasa wenye lengo la kujadiliana jinsi ya kuboresha daftari la kudumu la wapigakura watakaoshiriki uchaguzi mwaka 2020.
Jaji Kaijage ameongeza kuwa zoezi la uboreshaji daftari la wapigakura linaambatana na utoaji wa elimu kwa wananchi huku akitoa maelekezo kwa wale ambao wamehama katika maeneo yao ya makazi ya awali walipojiandikisha, kuharibu ama kupoteza kadi zao.