Wachezaji wa Bayern Munich
Akifanya mahojiano na Telegraph, Kimmich ameweka wazi kuwa kiwango cha Bayern msimu huu si kizuri tofuati na Liverpool hivyo lazima nafasi yao iwe ndogo katika mchezo wa leo.
"Liverpool ni timu bora kwasasa, huwezi kukwepa ukweli kwamba wamepoteza mchezo mmoja wa ligi mpaka sasa na wameruhusu goli 15 tu, lakini ukituangalia sisi hatupo kwenye wakati mzuri japo hii ni fursa ya kufanya vizuri na kurudi kwenye ubora'', amesema Kimmich.
Kimmich ameongeza kuwa pamoja na wao kuwa nyuma ya Dortmund kwenye msimamo wa Bundesliga lakini hawachezi vizuri, hivyo kama wachezaji wana wajibu wa kutumia mechi kama hii kufanya vizuri ili warudi tena kuwa timu bora Ulaya.
Joshua Kimmich
Pamoja na kutokuwa kwenye kiwango kizuri lakini Bayern ipo kwenye robo fainali ya Kombe la Ujerumani maarufu DFB-Pokal pia wapo 16 bora katika Ligi ya Mabingwa na leo saa 5:00 usiku wanacheza na Liverpool kwenye uwanja wa Anfield.
Kimmich mpaka sasa ndio mchezaji wa Bayern aliyetengeneza mabao mengi zaidi akiwa ametoa Assist 10 mpaka sasa sawa na wachezaji Eden Hazard wa Chelsea na Lionel Messi wa Barcelona.