Kikosi cha Yanga
Kiungo Feisal Salum maarufu 'Fei Toto' na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael hawatakuwa sehemu ya mchezo huo utakaopigwa CCM Kirumba kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.
Mratibu wa Yanga Hafidhi Salehe ameweka wazi kuelekea mchezo huo wa Jumatano Februari 20, ambapo pia amesema kikosi kimetua salama jijini Mwanza asubuhi ya leo tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo.
Kushoto ni Gadiel Michael na kulia ni Feisal Salum
"Tutawakosa Gadiel na Feisal ambao ni muhimu kwetu lakini wana kadi tatu za njano hivyo hatuwezi kuwatumia. Tumefika salama Mwanza na timu itafanya mazoezi leo jioni kwenye uwanja wa CCM Kirumba" amesema Salehe.
Mchezo dhidi ya Mbaop FC utakuwa ni wa 25 kwa Yanga msimu huu na bado inaongoza ligi ikiwa na pointi 58. Kwa upande wa Mbao FC huo utakuwa mchezo wao wa 27 na tayari wana pointi 36 katika nafasi ya 6.